8.5 C
New York

Chart| Tanzania kinara Afrika Mashariki kwa uhuru wa vyombo vya habari

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda uhuru wa vyombo vya habari kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa mwaka 2024, kwa mujibu wa ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa ya Reporters Without Borders (RSF)

Ripoti hiyo iliyotolewa Mei 3, mwaka huu inaonesha kuwa Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 143 kwa mwaka 2023 hadi nafasi ya 97 mwaka huu.

Kupanda huko kwa nafasi 46 ndani ya mwaka mmoja kunatokana na mafanikio makubwa ya kuimarika kwa mazingira ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kulinganisha na nchi zote za Afrika.

Kwa kushika nafasi ya 97 kati ya nchi 180 duniani, Tanzania imekuwa kinara wa nchi zote za Afrika Mashariki kwa uhuru wa habari mwaka huu.

Tanzania iko vizuri kwenye uhuru wa habari mbele ya Kenya (102), Burundi (108), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (123), Uganda (128), Sudani Kusini (136), Rwanda (144) na Somalia (145).

Utafiti wa RSF umeangalia masuala kadhaa muhimu, ikiwemo misingi ya kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa wanahabari na dhana ya kijamii na kitamaduni.

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia ameimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini kama sehemu ya Falsafa yake ya 4R.

Falsafa ya 4R ya Rais Samia inazingatia maoneo ya Reform (mageuzi), Reconciliation (maridhiano), Resilience (ustahamilivu) na Rebuilding of the nation (kujenga upya).

Serikali ya Raia Samia imefungulia magazeti yaliyokuwa yamefungiwa na kuimarisha mazingira ya waandishi wa habari na vyombo vya habari kufanya kazi zao nchini.

Tangu Rais Samia alipoingia madarakani, matukio ya vyombo vya habari kufungiwa, kupigwa faini, waandishi kukamatwa au kuuwawa wakiwa katika majukumu yao ya kazi yametoweka nchini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img