21 C
New York

Visual| Siku 100 za mzozo Gaza

Published:

Mwandishi Wetu na Mashirika

Leo Januari 14, 2024 zimetimia siku 100 tangu Kundi la Hamasi lilipoishambulia Israel Oktoba 7, 2023 na kusababisha mzozo mbaya katika Ukanda wa Gaza unaoendelea hadi sasa.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 25,000 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 76,000 wakijeruhiwa kutokana na mashambulio hayo.

Aidha, watu mioni 2.2 hawa uhakika wa chakula huku wengine milioni 1.9 wakiwa tayari wameyakimbia makazi yao.

Juhudi kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani za kutaka kustishwa kwa mapigano hayo zimeendelea kugonga mwamba. Umoja wa Mataifa umeshutumu na kusema kuwa hilo ni “doa juu ya ubinadamu wetu wa pamoja” huku Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akihakikisha kwamba “hakuna mtu” atakayeizuia nchi hiyo katika vita vyake vya kuliangamiza kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina. 

“Zimepita siku 100 tangu vita hivyo vya uharibifu vilipoanza, kuua na kuwafukuza watu huko Gaza, kufuatia mashambulizi ya kutisha ya Hamas na makundi mengine dhidi ya raia wa Israeli.

“Imekuwa siku mia moja ya shida na huzuni kwa mateka na familia zao,” amesema Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, Philippe Lazzarini.

SOMA PIA: https://gazetini.co.tz/2023/12/19/infographic-tunachofahamu-siku-74-za-mzozo-wa-israel-gaza/

Upande wake Netanyahu akiwa Tel Aviv, amesisitiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwa hakuna mtu atakayewazuia. “Hakuna mtu atakayetuzuia, wala Hague, wala mhimili wa uovu, wala mtu mwingine yeyote,” amesema Netanyahu.

Kauli ya Waziri huyo inakuja kama jibu kwa Afrika Kusini ambayo imeifikisha Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikiishutumu kwa kitendo cha mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img