8.3 C
New York

Makala| Elimu bora, Mazingira bora inavyolipa Muheza

Published:

Na Faraja Masinde, Muheza

“Hata sisi walimu tumejifunza kwamba tunapofundisha hatutakiwi kutumia dakika zote 45 darasani hapana, kuna muda wa kuwatoa wanafunzi nje ya darasa kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo,” anasema Shabani Churi, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Antakae iliyoko wilayani Muheza mkoani Tanga.

Shule ya Msingi Antakae yenye wanafunzi 410 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na walimu nane walioajiriwa na Serikali huku mwalimu wa darasa la awali akiwa akijitolea kwa kulipwa na wazazi.

Inatekeleza Mradi wa ECO SCHOOL mwaka 2022 unaofadhiliwa na Nature Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la kuhifadhi misitu asili Tanzania (TFCG).

Akizungumzia mradi huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kwezitu iliyoko wilayani Muheza mkoani Tanga, Shaban Churi, anasema kwamba kwanza ili shule iweze kupata mradi huo unaolenga kutunza mazingira lazima kwanza iweze kutimiza vigezo vya mradi huo.

“Kwanza lazima iwe na ECO Committee na uwe na mpango kazi, walipounfa kamati hiyo kuna walimu ambao walipata mafunzo ya mradi kwa siku tano na baada ya kurejea shuleni walitoa mrejesho kwa walimu.

“Baada ya mafunzo hayo kilifanyika kitu kinatwa Environmental Review ambapo hiyo inahusisha kuangalia vitu ambavyo vinakuwa namadhara katika mazingira yako, kama shule tuliandika wazo la mradi mdogo (Micro Project),” anasema Churi.

Kulingana na Churi, wao shuleni hapo kulikuwa na changamoto ya mmomonyoko wa udongo, ukataji wamiti katika jamii inayowazunguka, kushindwa kuhifadhi taka katika sehemu husika.

“Hapo ndipo tukajua kwamba kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kauandika wazo la kuomba mradi huo,” anasema Churi.

Kulingana na mwalimu huyo, wamebaini kuwa kuna faida nyingi kupitia mradi huo ambao wameupokea.

“Huu mradi una kitu kinaitwa IVAC ambayo ni Investgation, Vision, Action na Change ambapo hii walimu tumepewa mafunzo namna ya kuitumia.

“Maana kwamba mwalimu unapokuwa unafundisha haitakiwi dakika zote 45 ziishie zote darasani, badala yake unatakiwa uwatoe wanafunzi nje darasa ili wakafanye uchunguzi wenyewe na wakifanya hivyo watatengeneza maelengo ambayo ndiyo yatatusaidia kwamba ni hatua gani zichukuliwe ambazo zikichukuliwa tunatarajia kwamba tutapata mabadiliko ya tabia ambayo watoto wamefundishwa au wamefanya uchunguzi kuhusu hicho kitu.

“Kwa hiyo tusema huu mradi una faida kubwa kwa watoto, kingine ni kwamba unatufanya tuthamini mazingira yetu na tuyatunze mfano hapa shuleni kama kuna eneo lina mmomonyoko wa ardhi tunatakiwa tuyatunze ndiyo sababu shuleni kwetu tumepanda nyasi ili kuonekane ni kijani kwani mradi huu unataka mazingira yawe na mwonekano ambao hata mtu akipita anaona kabisa kuna kitu ambacho kina mvutia na anaweza kwenda kufanyia kazi katika mazingira yake,” anasema Churi.

Kichocheo cha kutunza afya

Anasema kuwa mradi huo umewafanya watathimini na kuchukua hatua juu ya kutunza afya bora kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kwezitu iliyoko wilayani Muheza mkoani Tanga, Shaban Churi.

“Kama mnavyoona kwamba ndani ya maeneo ya shule yetu kuna vibao ambavyo tumeweka kwamba wapi unatakiwa kuhifadhi taka na wapi hutakiwi kupita na maelekezo mengine, hivyo hata watoto wenyewe wamekuwa walimu na afya zao zimekuwa salama.

“Pia, umetufundisha namna ya kuwajali watoto, kwani unapokuwa unafandisha basi mtoto huyo anatakiwa apate kitu kilicholengwa kwamba apatiwe, sambamba na hayo hawa watoto wanaopata haya mafunzo wakimaliza shule wanakuwa ni mabalozi wazuri wa kutunza mazingira kwani muda mwingi huwa na mabunge yao yanayohusu utunzaji wa mazingira hatua itakayochochea jamii kutunza maingira vema,” anasema Churi na kuongeza kuwa mradi huo utasaidia kuibua fursa ya kiuchumi kwa wanafunzi hao pindi watakapohitimu masomo yao.

Anasema uwepo wa vibao vya maelekezo mbalimbali kumewasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi hao na kwamba kwa sasa wako katika mkakati wa kutengeneza njia maalumu ambazo wanafunzi hao watazitumia kupita.

Mbali na shule hiyo ya Antakae shule nyingine inayotekeleza mradi huowa miaka miwili ni Kambai huku tayari mwaka mmoja ukiwa umekatika hadi sasa.

Churi anasema tangu kuanza kwa mradi huo kumekuwa na mwamko mkubwa kwa watoto kwani wameweza kujua na namna ya kuthamini mazingira na viumbe hai ikiwamo kuwatunza.

“Wengi wa wanafunzi wetu kwasasa wanafanya uangaliaji wa ndege ndani ya hifadhi ya Amani pamoja na hilo limewaelimisha juu ya kutambua thamani ya viumbe hai.

“Pia, mazingira yetu yameimarika, hivyo imeongeza usafi na hadhi ya shule tofauti na zamani ambapo watoto walikuwa wakitupa taka mahala popote pale,” anasema Churi.

Muundo wa Kamati ya ECO SCHOOL

Akizungumzia mwitikio wa wazazi, Churi anasema kuwa tangu kuanza kwa mradi huo wananchi kupitia kwa Mwenyekiti wa Kijiji alikuwa akishiriki vikao hivyo vya ECO SCHOOL ambapo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kujenga uelewa.

“Kamati hii ya mradi huu inakuwa na mwalimu mkuu kama Kiongozi, Mwalimu wa Mazingira, Wajumbe wawili kutoka umoja wa walimu na wazazi, mjumbe mmoja kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanne.

“Wakati wa mafunzo tulijifunza kwamba ukichagua mradi ambao utakuwa hai basi wenywe utaweza kuwa endelevu hata baada ya kipindi cha mradi kilichopangwa kuisha.

“Ukingalia miradi kama ya ufugaji kuku ilikuwa haishauriwi sababu sehemu kubwa ya watu waliowahi kufanya mradi wa namna hii hawajawahi kufanikiwa, hivyo kwa hiki tulichochagua hata mradi ukifikia ukingoni bado tunaweza kuendelea na mradi wetu,” anasema Churi.

Ikumbukwe kuwa mradi huo unaotekelezwa na TFCG na Nature Tanzania kupitia shule unafadhiliwa na USAID kupitia mradi wa Tuhifadhi Maliasili.

Mmoja wa Wanafunzi, Mwajuma Hassan anayesoma darasa la tano shuleni hapo anasema kuwa: “Mazingira mazuri ya shule ni jukumu letu sote kuhakikisha kwamba tunasoma tukiwa salama, tunajitahidi kumuelimisha kila mmoja anayetembelea shuleni kwetu kuhakikisha kwamba anajifunza kuhusu kutunza mazingira na kudhibiti utupaji taka ovyo,” anasema Mwajuma.

Samweli Allen ambaye ni Afisa Mafunzo Msaidizi kutoka Nature Tanzania, anasema kuwa mradi huo hautekelezwi Muheza tu bali unatakelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo mikoa ya Morogoro na Lindi lengo likiwa ni kusaidia shule kupata bendera ya kijani (Green Fly) kwa kufanya vizuri katika mazingira.

“Huwa tunawasisitiza sana kwamba hata kama mradi utaisha basi wao wanatakiwa kile wanachokitekeleza kwasasa kiendelee kuwepo ili hata baadae wakiandika wazo wa mradi jingine wanaweza kuwezeshwa,” anasema Allen.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img