4.2 C
New York

Infographic| Mafanikio yaliyofikiwa uzalishaji maji nchini

Published:

Kwa miaka ya karibuni sehemu kubwa ya miji ya Tanzania imeendelea kupata huduma muhimu ya maji.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia MUHTASARI WA PATO LA TAIFA
(APRILI – JUNI) ROBO YA PILI 2021,inabainisha kuwa kumekuwa na ongezeko katika uzalishaji maji nchini.

Hiyo inahusisha kukusanya na kusafisha maji kwa ajili ya ugavi wa maji,kusafisha maji ya bahari kwa kuondoa chumvi ili kuweza kuzalisha maji ya kutumia kama bidhaa kuu na kukusanya maji moja kwa moja kutoka katika visima kwa ajili ya matumizi ya makampuni ya maji au matumizi binafsi katika kilimo au kaya.

Aidha, shughuli hii pia inahusika na ukusanyaji wa maji taka.
Kwa mujibu wa NBS kiashiria cha kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa shughuli ya usambazaji majini kiasi cha maji kilichozalishwa. Katika robo ya pili ya mwaka 2021, kiasi cha maji kilichozalishwa kiliongezeka hadi mita za ujazo milioni 81.6 kutoka mita za ujazo
milioni 74.7 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Shughuli ya usambazaji maji ilikua hadi asilimia 8.4 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2021 kutoka asilimia 4.6 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Sababu zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na kuendelea kuboreshwa kwa miundombinu ya uzalishaji maji kwa lengo la kuongeza uwezo wa uzalishaji na kuendelea kuzalisha maji zaidi ili kukidhi mahitaji ya maji ambayo yanaendana na ongezeko la idadi ya watu hususani katika maeneo ya mijini.

Zaidi angalia chati yetu kuona ongezeko hilo la uzalishaji maji kuanzia mwaka 2016 hadi 2021.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img