23.3 C
New York

Wizara ya Fedha yaoamba Sh 20.19  trilioni,  deni la Serikali  10.19 trilioni zimelipwa

Published:

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, ameliomba Bunge la  Tanzania kuidhinisha Sh 20.19  trilioni kwa ajili ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Mapema leo Juni 4, 2025, Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba, aliwasilisha bungeni  jijini Dodoma mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2024/25 na mapendekezo ya mpango na bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26.

Kati ya fedha hizo, Sh19.43 trilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 757.79 bilioni ni matumizi ya maendeleo, na jumla ya  Sh 122.52 bilioni ni kwa  ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Dk. Nchemba amesema fedha hizo zitawezesha kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kutafuta na kukusanya mapato ya jumla ya shilingi trilioni 50.98, kuhudumia kwa wakati deni la Serikali linalotarajiwa kuiva la sh 14.22 trilioni  na kuandaa sera ya usimamizi wa mali za umma.

Amesema kati ya fedha hizo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kukusanya jumla ya Sh 34.10 trilioni, misaada Sh 1.07 trilioni,  mikopo nafuu na ya kibiashara kutoka vyanzo vya ndani na nje Sh 14.95 trilioni na maduhuli  Sh 53.54 bilioni .

Aidha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inakadiriwa kukusanya  Sh  843 milioni , ikiwa ni ukodishaji wa kumbi za mikutano na kodi ya pango kutokana na upangishaji wa majengo ya ofisi yaliyopo katika mikoa mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine  Waziri Nchemba amesema   deni la Serikali limeendelea kuhudumiwa kufikia Aprili, 2025 ambapo jumla ya Sh 10.19  trilioni zimelipwa kwa notisi za madai ya deni lililoiva, sawa na asilimia 84.8 ya lengo la mwaka.

“Kati ya kiasi hicho, jumla ya malipo ya deni la ndani ni shilingi  trilioni 6.01, ikijumuisha  riba shilingi trilioni 2.48 na mtaji shilingi trilioni 3.53 na deni la nje ni shilingi trilioni 4.18, riba ikiwa ni shilingi trilioni 1.62 na mtaji shilingi trilioni 2.56,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img