Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kimya cha muda mrefu, staa wa Bongo Fleva Yakuti Joseph a.k.a YJ Kiboko ameibuliwa upya na kolabo yake na mkongwe wa muziki huo Dully Sykes.
Wawili hao wameachia kolabo ya wimbo wao unaoitwa Mama Yoyo ambao ndani ya muda mfupi umewakosha
wapenzi wa muziki huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza na Habari Leo, YJ Kiboko amewashukuru mashabiki kwa mapokezi ya ‘Mama Yoyo’ ambayo amepewa heshima na mwanamuziki mkongwe Dully Sykes kuonyesha makali yake.
“Upendo wa mashabiki ni mkubwa sana, Mama Yoyo inatembea vibaya mno kwenye mitandao ya kijamii, huko club ni balaa ndio ngoma inayochezwa kwa wingi kipindi hiki,” amesema YJ Kiboko.