22.6 C
New York

Dj Davizo awashtua mashabiki

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini


Staa wa Bongo Fleva kutoka Bunduki Music, Dj Davizo, amewashtua mashabiki punde baada ya kuachia wimbo wenye vionjo vya gospo, Prayer.

Davizo, amejizolea umaarufu Bongo kwa ngoma zake kali zinazowapa raha mashabiki kwenye klabu za burudani lakini amebadikisha upepo ghafla baada ya iuachia audio na video ya wimbo Prayer.

Akizungumza na gazetini.com, Davizo amewashukuru mashabiki zake kwa mapokezi ya ngoma hiyo Prayer ambayo imeendelea kutoa picha ya ukubwa wa kipaji cha Dj huyo.

“Prayer ni ngoma ya maombi wa Mungu, katikati ya maisha yetu ya ujana mwingi tusisahau kufanya sala na dua ili tuzidi kufanikiwa, kuanzia sasa wimbo wangu Prayer inapatikana katika mitandao yote ya muziki kama YouTube na nyingine, mashabiki waendelee kusapoti kazi nzuri,” amesema Davizo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img