21.1 C
New York

Sakata lake na Harmonize, Ibraah ashusha pumzi Basata

Published:

Na Mwandishi Wetu

Baada ya kutoka ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Abdallah ‘Ibraah’, amesema ishu yake Konde Gang Music imefika kwenye mikono ya walezi, hivyo kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu hiyo ni Serikali itaangalia wapi kuna haki na sheria itafuata mkondo wake.

Ibraah amefika Basata leo Mei 12, 2025 kuitika wito wa baraza hilo kutokana na sakata linaloendelea kati ya na lebo Konde Gang baada ya kutangaza kutaka kujitoa ambapo waliitwa yeye na Harmonize ambaye hakutokea.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa nimefika kwenye mikono ya walezi wetu, nadhani soon litakuwa sawa kwa sababu limefafika nyumbani,” amesema Ibraah.

Msanii huyo amekuwa kwenye mvutano na uongozi wa lebo hiyo Konde Gang Music Worlwide ambao jana Mei 11,2025 ulitangaza kumsimamisha Ibraah kushiriki shughuli zozozte za muziki hadi pale suala lake litakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa mijibu wa mkataba wake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img