13.9 C
New York

Mnyama anawacheki tu hapo kileleni, bado pointi 4

Published:

Na Mwandishi Wetu

Simba imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo Mei 8,2025 kwenye Uwanja wa KMC Complex, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo mabao ya Simba yamefungwa na Jean Ahoua alifunga matatu ‘Hat trick’ na Lionel Ateba aliyefunga mawili, huku bao la Pamba likifungwa na Mathew Momanyi.

Ushindi huo unaifanya Simba kupunguza ‘gap’ la pointi ambapo imebakisha alama nne kuifikia Yanga iliyopo kileleni na pointi 70.

Simba imefikisha pointi 66 ikiwa imecheza michezo 25, wakati Yanga imecheza mechi 26.

Kwa upande wa Pamba hali inazidi kuwa ngumu kwao, kwani ipo katika hatari ya kushuka daraja ambapo inashika nafasi ya 13 katika msimamo na pointi 27, imecheza michezo 27.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img