18.7 C
New York

Salum Mwalimu, wanachama wengine watangaza kujitoa Chadema, wasema wao sio chawa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu  wa Chadema  Zanzibar, Salum Mwalimu na wanachama wengine wa chama hicho wametangaza kujitoa  katika chama hicho  kwa madai ya kutoridhishwa na yanayoendelea.

Wametangaza uamuzi huo leo Mei 7, 2025 jijini Dar es wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Akitangaza uamuzi huo  aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Benson Kigaila akiwa pamoja na Salumu Mwalimu, aliyewai kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake  (Bawacha), Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita, amesema wamejitoa lakini hawaendi CCM.

Kigaila amesema muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia  na sasa wanashauriana na vyamba mbalimbali.

“Sisi tumeamua wote  kwa pamoja kujiondoa Chadema ili tuwaachie hicho chama waendeshe wanavyotaka. Hatuwezi kuwa  wanachama wa chama ambacho maamuzi yake hayafanywi kwa vikao.

“Hatuwezi kuwa wanachama ambao wanabaguliwa.Katiba haifuatwi, sisi sio chawa, sisi tunajitambua, tuliingia Chadema malengo na tunatoka Chadema kwa sababu malengo yameisha basi tunawaachia chama chao,” ameelaza Kigaila.

Kwa upande wake Mwalimu amesema  alikuwepo katika chama hicho kwa muda mrefu na hakufuata vyeo wala fedha bali aliamini kwamba kama mtoto wa Taifa hili ana kila sababu ya kutoa mchango wake nchini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img