24.4 C
New York

‘Mawinga’ matapeli mtandaoni kudhibitiwa, serikali yavuna mabilioni kwenye kubeti

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Serikali imekiri kuwepo kwa ujanja ujanja katika biashara ya mtandaoni, hivyo imeanza kuchukua hatua na kupunguza changamoto hiyo kwa kuwa na  mkakati wa Kitaifa wa biashara hizo.

Hayo yameelezwa leo  Aprili 29,2025 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Ritta Kabati, lilihoji  ni upi mkakati wa serikali kudhibiti utapeli na udanganyifu kwenye biashara mtandao?

“Ni kweli kuna changamoto ya biashara ya kuuza bidhaa mtandaoni bila kuwa na kampuni, Kwa mfano mtu anapiga picha bidhaa mtu dukani harafu anarusha mtandaoni, anatafuta wateja. Sasa mtu akama hujui ameweka na namba ambayo  bado ukituma hela mzigo hutapata na fedha yako imekuwa imetapeliwa.

“Mikakati mengine, Serikali kupitia wizara mbalimbali, Mfano kupitia, Wizara ya Fedha, tayari wana kitengo mahususi ambayo inasimamia biashara mtandaoni,” amefafanua Kigahe.

Ameongeza kuwa, sheria mbalimbali zimeendelea kuundwa Mfano Sheria ya Usalama wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na sheria nyingine.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali imekusanya Sh 192.78 bilioni kutoka kwenye biashara mtandao ikihusisha michezo ya ubashiri(kubeti) katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi mwaka huu kutoka kwa kampuni 1820 za biashara mtandaoni ambayo tayari zimeshasajiliwa.

Amesema serikali imepanga kuchukua hatua muhimu za kuwa na mfumo madhubuti utakaosimamia biashara hiyo ili kwenda sambamba na mfumo wa mabadiliko ya kiteknolojia pia kukusanya mapato zaidi.

Kigahe ameeleza hayo wakati  akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Ritta Kabati, lilihoji iwapo serikali inatambua biashara ya mtandao na makampuni mangapi yamejisajili na mapato kiasi gani yamepatikana kwenye biashara hiyo.

“Mhe. Mwenyekiti, ili kuhakikisha tunaenda sambamba na mabadili hayo, serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Biashara Mtandao ‘National Electronic Commerce Stratergy’ ambao upo kwenye hatua za mwisho za utekelezaji wake,” amefafanua Kigahe.

Amesema maeneo yatakayofanyiwa kazi kwenye utekelezaji wa mkakati huo ni uboreshaji wa miundombinu ya (TEHAMA), uboreshaji wa sera, sheria na kanuni, uboreshaji wa huduma za mawasiliano, usafirishaji na uchukuzi, uimarishaji wa huduma za miamala kwa njia ya mtandao na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu na biashara mtandao ili kutumia majukwaa mtandao yaliyopo kufanya biashara.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img