Na Winfrida Mtoi, Gazetini
Mashindano ya kuogelea ya Klabu Bingwa Taifa yameanza huku uongozi wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), ukiwa na matumaini makubwa ya kupata waogeleaji bora watakaiwakilisha Tanzania katika michuano mbalimbali ya Kimataifa mwaka huu.
Michuano hiyo ya siku mbili inatanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) ambapo zaidi ya waogeleaji 100 wanashiriki.
Akizungumzia mashindano hayo,, Mwenyekiti wa (TSA), David Mwasyoge, ushindani ni mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji na kila mmoja akitaka kuvunja rekodi.
“Haya ni mashindano ambayo yanaangalia zaidi ubora, hata wachezaji walioshiriki ni wale wenye viwango vya juu. Ushindani ni mkubwa na kadiri wanavyozidi kuvunja rekodi ina maana wapo tayari kushiriki Kimataifa,” amesema.
“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunafuvu katika mashindano makubwa. Hawatakiwi kubweteka bali kuendelea kupambana,”
Kwa upande wake mchezaji Collins Saliboko, amesema kuna mashindano makubwa ya Kimataifa yakuja, hivyo atatumia michuano hiyo kujiweka sawa na kujua ni kitu gani anatakiwa kurekebisha.