11.1 C
New York

Mwenyekiti wa CCM Rorya adaiwa kugawa viongozi wa chama, watendaji

Published:

*Kada wa CCM amuomba Wasira washuke kuona yanayoendele, Mwenyekiti Ongujo atoa kauli

Na Mwandishi Wetu, Rorya

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka wilayani Rorya mkoani Mara, Baraka Otieno amekiomba  chama hicho kuunda chombo maalumu cha kuchunguza mwenendo wa kisiasa unaoendelea wilayani humo.

Ombi hilo linatokana na uwepo wa taarifa zinazomtuhumu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Rorya,  Ongujo Wakibara pamoja na mbunge wa jimbo hilo Jafari Chege kuwa wamekuwa wakikivuruga chama hicho kwa masilahi yao binafsi.

Akizungumza leo Februari 25, 2025 Jijini Dar es salaam waandishi wa habari Otieno amedai viongozi hao wamekuwa wakitumia fedha na nafasi zao kuvunja katiba ya chama hicho na kuondoa utulivu uliopo.

Akieleza zaidi Februari 21, mwaka huu chama hicho taifa kiliandaa mafunzo maalumu kwa watendaji wa chama ngazi ya tawi na kata kwa gharama za chama lakini cha kusikitisha viongozi hao walitoa fedha Shilingi 50,000 kwa kila mjumbe aliyeshiriki mafunzo hayo hali ambayo imetafisiliwa kuwa ni rushwa.

“Nipo hapa kwa ajili ya kukilinda kukeme na kueneza chama hiki kwani chama hiki kwakuwa kinaaminiwa na watanzania na ndio maana kinapewa dhamana ya kuongoza nchi hivyo nimewaiteni hapa ili nitoe  tamko kuhusu vitendo hivi vya kustajabisha vinavyotokea rory mkoani mara.

“Mimi sio tu kada wa chama cha mapinduzi kama mnavyojua lakini ni mtu ambaye nimefanya kazi makao makuu katika idara ya siasa uhusiano wa kimataifa hivyo chama hiki ninakifahamu .Nina uhakika ninapokizungumzia chama hiki pamoja na mambo mengine ninagusa moja kwa moja mstakabali wa taifa,” alisema Otieno. 

Kutokana na hali hiyo aliongeza kuwa kupitia mafunzo hayo chama makao makuu kilitoa maagizo na maelekezo kwamba wabunge na wadau wengine hakuna kutoa kitu fedha kwani gharama hizo zilibebwa na chama.

Amesema chama kilifanya hivyo kwasababu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kwakutambua unyeti wa mafunzo hayo na kukwepa watu wengine kuyatumia mafunzo hayo kwa maslahi binafsi katibu mkuu alitoa maelekezo muhimu kwa watendaji.

Kada huyo amesema miongoni mwa maelekezo hayo ilikuwa ni marufuku wa mtu yeyote awe mbunge wa jimbo au mtarajiwa au mdau yeyote kujihusisha  na mafunzo hayo.

Otieno amesema kwa upande wa rory kuna mwenyekiti wa chama hicho wilaya akishirikiana na mbunge wa jimbo hilo walivuruga mafunzo hayo kwani waliingilia  na kugawa rushwa ya fedha ya Shilingi 50,000 kwa wajumbe kinyume na maagizo.

Ameongeza kuwa mwenyekiti huyo wa chama wilaya amekuwa akitangaza hadharani kuunga mkono mbunge wa sasa Jafar chege nakwamba hiyo nikinyume na Katiba ya CCM inayomtaka yeye kama kiongozi mkuu wa chama na baba wafamilia na wana CCM wote ndani ya wilaya kutojihusisha na kundi lolote lile.

“Hapa tulipo hatufanyi siasa za maji taka bali tumekuja na ushahidi clip mbalimbali  na katika vikao na mikutano mbalimbali amekuwa akitangaza wazi wazi kumuunga mkono mbunge wa sasa na huyu Mwenyekiti wa CCM Wilaya amekuwa akitoa maelekezo ya kuwasimamisha na kuwafukuza viongozi wa mashina,tawi na kata ambao hamuungi mkono mbunge wa sasa na baadhi ya madiwani,” amesema.

Pia amedai mwenyekiti huyo amekuwa akiwatishia madiwani na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa atakata majina yao kama hawatamuunga mkono mbunge wa sasa na ushahidi upo.

Amesema viongozi hao wamekuwa na tabia ya kuwabagua viongozi wa matawi na kata ambao hawako upande wao hivyo wao kama makada hawawezi kamwe kunyamazia vitendo hivyo.

Otieno amesema Mwenyekiti huyo amekuwa akiwaagiza viongozi wa chama ngazi ya kata kuwasimamisha viongozi wa matawi pasipokufuata katiba na bila kuhusisha kamati ya siasa ya wilaya.

“Kutokana na maelezo haya ndio maana tunashauri au kuomba chama kuunda chombo maalumu kitakacho fuatilia haya yote na kuchukua hatia dhidi ya mwenyekiti na mbunge .wanaccm wa rory wanakipenda sana chama chetu lakini haya yanayofanywa na mwenyekiti yanasababisha chama kichukiwe,” amesema.

Akijibu tuhuma hizo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ongujo Wakibara amesema tuhuma zinazotolewa na kada huyo hazina mashiko wala ukweli wowote na kinachoendelea hapo ni vita vya ubunge.

Amesema kuhusu madai ya kutoa fedha kwa wajumbe ni hoja ambayo haina msingi wowote na wala sio vibaya kutoa asante kwa mtu ambaye anafanya vizuri na hilo linafanyika na yeye ni mwenyekiti wa chama na amekuwa akishiriki katika matukio mbalimbali.

“Kwanza siku ambayo kulikuwa na mafunzo kwa watendaji mbunge alikuwa msibani na mimi nilifika ukumbini mwishoni kuwasalimia watoa mafunzo. Mimi ndiyo msimamizi wa chama ngazi ya Wilaya na ndiyo msimamizi wa utekelezaji wa ilani,” amesema

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img