1.4 C
New York

Chart| Miundombinu shuleni bado changamoto

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Pamoja na jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo la upungufu wa miundombinu ya elimu katika shule ikiwamo kujenga majengo mapya na kukarabati vyumba vya madarasa kwa shule zenye msongamano wa wanafunzi, hali inaonyesha bado kuna kazi ya kufanya.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), tathimini ya utoshelevu wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari iliyofanywa na ofisi ya CAG ilibaini kuwa mamlaka 18 za Serikali za Mitaa zilikuwa na upungufu wa miundombinu mbalimbali.

Athari za upungufu huo ni pamoja na kuwapo kwa msongamano katika madarasa na mabweni, uwiano usiosawia wa vyoo kwa idadi ya wanafunzi, pamoja na uhaba wa viti, meza na madawati hatua inayoathiri mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Aidha, uhaba wa nyumba za walimu, ofisi na samani huathiri mazingira ya kufundishia, jambo linalokwamisha ufaulu wa wanafunzi.

Katika ripoti hiyo, CAG amependekeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, itoe fedha kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa ili kuondoa au kupunguza uhaba wa miundombinu.

Pia, wahakikishe wanaweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa elimu bora. Zaidi angalia usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img