8.7 C
New York

Hii ni Afrika: Onesho la sanaa ya muziki wa majukwaa linalolenga kufufua sanaa hiyo Tanzania

Published:

*Ni onesho linalolenga kufufua, kurejesha na kupeleka sanaa ya majukwaa ya Tanzania kimataifa

*Litafanyika Agosti 12 na 13, 2023 katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam

*Litawakutanisha pamoja wadau wa maendeleo, sanaa, Utamaduni na muziki

Na Tulinagwe Malopa, Gazetini

Huenda sanaa ya Muziki na Maigizo ya majukwaa Tanzania ikafufuka na kuimarika kwa kasi siku za usoni, baada ya wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na Bodi ya Filamu Tanzania kuungana kwa pamoja kuandaa onesho la sanaa ya muziki wa majukwaa mwishoni mwa wiki hii.

Onesho hilo lililopewa jina la Hii ni Afika linalenga kufikia takribani watu 2,000 ili kufufua, kurejesha na kupeleka sanaa ya majukwaa ya Tanzania kimataifa kupitia kukuza vipaji vya vijana wanaochipukia katika tasnia ya sanaa.

Onesho hilo linalosimamiwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Bora Initiative (TBI) kwa kushirikiana na Serikali, na wadau mbalimbali wa sanaa Tanzania linatarajiwa litafanyika Agosti 12, 2023 na kumalizika Agosti 13, 2023.

Onesho hilo litafanyika kwa njia ya jukwaa katika Makumbusho ya Taifa ya Tanzania jijini Dar es Salaam kuangalia vipaji vya waigizaji, wacheza dansi, waimbaji, wanamuziki na washairi 60 walioshiriki kuandaa onesho hilo.

Mwanzilishi wa Tanzania Bora Initiative, Abella Bateyunga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono juhudi zao kama wadau ili kufikisha Tanzania katika viwango vya Kimataifa kwenye sanaa ya majukwaa

“Tunashukuru Serikali, mabalozi na wadau mbalimbali kwa kutuunga mkoni juhudi zetu za kufufua na kuimarisha michezo hii. Tunayo kiu michezo ya kuigiza na michezo ya majukwaa kurudi Tanzania,” amesema Abella.

Kwa upande wake, Dk. Kiagho Kilonzo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania ametoa wito kwa wasanii kuanzia katika maigizo ya majukwaa, amesema wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa jitihada zinazofanywa na wadau kukuza tasnia ya sanaa nchini.

“Ili uwe mwigizaji mzuri wa filamu lazima uanie jukwaani. Sisi tupo kuunga mkono hatua kama hizi ili kukuza tasnia ya sanaa Tanzania,” amesema Dk. Kilonzo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img