22.9 C
New York

Visual| Fahamu idadi ya Watoto Tanzania

Published:

*Serikali iongeze nguvu vijijini

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Kulingana na matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya Watoto nchini Tanzania ni 32,682,377.

Matokeo hayo yanadhihirisha usemi usiemao kwamba watoto ndiyo taifa la kesho, kwani kulingana na matokeo hayo yaliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) mwaka 2023 yanaonyesha kuwa kundi hilo la watoto wenye umri kati ya mwaka 0 hadi miaka 19 ni asilimia 52.93% ya watu wote nchini Tanzania.

Kiwango hicho ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote.

Aidha, matokeo hayo ya NBS yanaonesha kuwa idadi ya watoto walioko vijijini ni kubwa ikilinganishwa na wale waliko mijini.

Kulingana na matokeo hayo, watoto waliko vijijini ni 22,476,852 huku wale walioko mijini wakiwa ni 970,499. Hii ni sawa na kusema kwamba watoto waliko maeneo ya vijijini ni mara 23 ya wale walioko mijini.

Hivyo basi, Serikali haina budi kuhakikisha kwamba inatilia mkazo huduma bora kwa maeneo ya vijini ambako ndiko kundi kubwa la watoto liliko ikiwamo kuimarisha miundombinu ya elimu, huduma bora za afya, maji safi, umeme na nyanja nyingine muhimu bila kusahau wale wa mijini.

Kwani kwa sehmu kubwa ya miundombinu hasa ya elimu katika maeneo mengi yaliyoko vijini bado siyo rafikir kwa wanafunzi kwa kiasi kikubwa hii ikiwa ni pamoja na umbali wa shule na huduma nyingine.

Pia kulingana na matokeo hayo, kundi la watoto wenye umri kati ya mwaka 0 hadi 4 ndilo linaongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi ikilinganishwa na makundi mengine ya Watanzania katika matokeo hayo ya sensa.

Matokeo yanaonyesha kuwa kundi hilo lina jumla ya watoto milioni 9.48 likifuatiwa na kundi la watu wenye umri wa miaka 5 hadi 9 ambao ni milioni 8.91.

Zaidi angalia #Usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img