21 C
New York

Visual| Tanzania na mkakati wa kudhibiti Malaria 2030

Published:

Na Jackline Jerome, Gazetini

Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa katika kuhakikisha ugonjwa wa Malaria unadhibitiwa huduma za ugonjwa huo zitaanza kutolewa bure katika vituo vya afya nchi nzima.

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa Aprili 25, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Ugonjwa huo Duniania.

Akizungumza Aprili 25, katika Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Kitaifa jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu Majaliwa alimwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Ikumbukwe kuwa lengo la Tanzania ni kuhakikisha kuwa inatokemeza ugonjwa huo ifikapo 2030.

Waziri Mkuu alisema nini?

Majaliwa alisema kuwa: “Kutokana na kutoa wito wa kupunguza malaria nchini, wananchi watapata huduma bureikiwamo vipimo vya malaria, sindano kali, dawa ya ASP hizi huduma zote zitatolewa bure katika vituo vyetu vyote vya afya,” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa ameagiza viongozi wa Serikali za Mitaa kuwahimiza wananchi kuwa kuanzia sasa kuwa ni marufuku kutumia chandarua chenye dawa kwa ajili ya malaria kuweka kwenye bustani za mboga.

Amesema licha ya maambukizi ya malaria kupungua bado vifo vinaendelea kutokea vinavyosababishwa na ungonjwa huo, ambapo takwimu zinaonyesha mwaka 2015 ilikuwa asilimia 14.8 hadi sasa umepungua hadi asilimia 8.1 huku akitaja mikoa kinara.

“Mikoa inayoongoza kwa maambukizi dhidi ya malaria ni Tabora 23%, Mtwara 20%, Kagera 18%, Shinyanga 16% na Mara 15%. Tunahitaji kutokomeza malaria tunapoteza nguvu kazi ya Taifa,” amesema Majaliwa.

Sambamba na hayo, Serikali imeipongeza mikoa yote tisa ambayo imeweza kutokomeza malaria ikiwemo Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Songwe, Njombe, Manyara, Singida na mingineyo.

Waziri wa Afya

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema 94% ya Watanzania wapo hatarini kupata ugonjwa wa malaria na vinashuhudiwa vifo vinavyotokana na malaria na kwamba ugonjwa huo bado ni tishio.

Amesema takwimu zinaonyesha maambukizi ya malaria nchini yamepungua kwa asilimia 50.

“Pamoja na mapambano yanayoendelea kuna uhaba karibu 57% wa rasmali kwa ajili ya kutekeleza mpango mkakati wa malaria wa mwaka 2021 hadi 2025,” amesema Ummy.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti (NIMR), Dk. George Praygod anasema wamepunguza vifo vya malaria kwani katika miaka ya 2000 walikuwa na wagonjwa zaidi ya 100,000 sasa wana vifo chini ya 10,000 ambayo ni mafanikio.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img