1.4 C
New York

Ripoti| Wafanyakazi wengi wanatishwa kazini Tanzania

Published:

Machapisho mbalimbali yanaitafsiri Kazi kama ni seti ya shughuli ambazo zinafanywa kwa ajili ya kufikia lengo, kutatua shida au kuzalisha bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya binadamu.

Aidha, neno kazi linatokana na Kilatini utatu, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na kwa zamu ya safari tatu, ambayo ilikuwa aina ya nira ya kuchapwa watumwa katika Dola ya Kirumi.

Kwa muda, matumizi ya neno hilo yaliongezeka kumaanisha shughuli ambayo ilisababisha maumivu ya mwili na ilihusishwa na kufanya kazi mashambani, lakini matumizi yake yalisambaa kwa shughuli zingine za kibinadamu.

Inafafanuliwa kama utendaji unaotumia nguvu ya akili au ya mwili ili kufikia lengo fulani, ambalo mara nyingi ni faida ya kiuchumi ili kuweza na kuwezesha kuendelea kuishi.

Kwa msingi huo, ni wajibu wa kila mtu aliyefikia ukomavu fulani. Ni pia ina mchango muhimu katika jamii na inayostahili kuheshimiwa na kutunzwa na wote kuanzia serikali hadi watu binafsi. Kwa kuwa ni wajibu, kazi ni vilevile haki ya msingi ya binadamu.

Bila kuwa nayo, mtu anaelekea kunyong’onyea na kujiona hana maana, hasa kama utovu wa kazi unadumu muda mrefu na kumzuia asiweze kupanga maisha yake, kwa mfano upande wa ndoa na familia, kwa sababu ya kutojitegemea.

Aidha, kumekuwapo na sheria mbalimbali zinazoratibu mahusiano kazini, hasa kama kuna mwajiri na mwajiriwa. Kama hiyo haitoshi kumekuwa na Wakala wa kuangalia usalama na afya mahali pa kazi kwa maana ya (OSHA).

Hata hivyo, nchini Tanzania baadhi ya sehemu za kazi bado zimejawa na changamoto lukuki huku kubwa ikiwa ni ile ya kutishwa.

Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadumu(LHRC) ya mwaka 2020/21 kuhusu Haki za Binadamu na Biashara inabainisha kuwapo kwa mazira makubwa yanayowapata wafanyakazi wawapo kazini.

Ripoti hiyo imeonyesha namna ambavyo matukio ukatili na unyanyasaji, hasa kwa wanawake na watoto, yamekuwa mwiba mkubwa kwa haki za binadamu. Matukio hayo hutokea katika sehemu mbalimbali, ikiwemo majumbani, mitaani, mashuleni na hata mahala pa kazi.

Kwa mujibu wa LHRC, Utafiti kuhusu haki za binadamu na biashara ulilenga kutambua kama kuna aina zozote za ukatili na unyanyasaji mahala pa kazi zilitokea katika kipindi cha 2020/2021.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa takribani theluti moja ya wafanyakazi (29%) walidai kwamba kumekuwa na matukio ya ukatili na unyanyasaji mahala pao pa kazi, huku 71% wakisema kwamba hakuna matukio hayo.

“Hata hivyo, pamoja na wafanyakazi wengi kudai hakuna matukio ya ukatili na unyanyasaji mahala pao pa kazi, utafiti uligundua kwamba mtazamo huu unaweza kuwa unasababishwa na uelewa wao mdogo kuhusu ukatili na unyanyasaji, kana kwamba kunaweza kuwa na matukio yanatokea ila wao hawajui kama ni ya ukatili au unyanyasaji.

“Mathalani, wafanyakazi wengi waliohojiwa walidai kutishiwa kwa namna mbalimbali, kitendo ambacho ni cha ukatili pia.

“Wafanyakazi waliodai kuwepo kwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji mahala pao pa kazi walitambua aina mbalimbali za vitendo vya ukatili na unyanyasaji, ambapo wengi wao (73%) walitaja vitisho na kuonewa kama aina ya ukatili na unyanyasaji inayotokea zaidi mahala pao pa kazi, wakifuatia na waliodai vitendo vya ukatili wa kingono (15%),” Inabainisha Ripoti hiyo.

Aidha, aina nyingine ya ukatili na unyanyasaji ambao hutokea zaidi kazini ni Shambulio la mwili (6%) na mwingine (65).

Hii ni sawa na kusema kwamba wafanyakazi wengi nchini wanatishwa kwenye maeneo yao ya kazi.
Ni wazi kwamba Serikali inahaja ya kuangalia baadhi ya sera kwani katika ofisi nyingi zinazomilikiwa na baadhi ya raia wa kigeni hasa wanaotoka Bara la Asia ambapo wamekuwa wakilalamikiwa kwa kufanya vitendo visivyofaa kwa wafanyakazi wao.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img