1.4 C
New York

Infographic| Hali ya maambukizi ya VVU nchini

Published:

Akichambua ripoti ya utafiti uliofanyika juu ya maambukizi ya VVU Tanzania (Tanzania HIV Impact Survey) 2016-2017, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lucas Shija Kitula, anasema hali ya upimaji wa VVU nchini bado ni panda shuka na kwamba jitihada za makusudi za kutoa elimu zinahitajika.

Kwa mujibu wa Kitula, asilimia 29.2 ya wanawake wenye umri wa miaka 15 na kuendelea hawajawahi kupima VVU huku kiwango kikiwa kikubwa zaidi kwa wanaume wenye umri sawa na huo ambao ni asilimia 40.8.

“Lakini pia tukija kwenye upande wa umri wa vijana ni miaka 15 hadi 19 hali ya upimaji nako bado siyo ya kuridhisha.

“Kwani wavulana ambao hawajawahi kupima VVU ni asilimia 79 huku upande wa wasichana wakiwa ni asilimia 61.4.

“Upande mwingine tunaona kuwa elimu imekuwa na msaada kwani takwimu zinaonyesha kuwa upimaji wa VVU kwa watu wenye elimu ya chuo kikuu ni asilimia 89.3 ikilinganishwa na asilimia 54.4 ya wale ambao hawajasoma,” anasema Kitula.

Wenye maambukizi

Kitula anaendelea kufafanua zaidi kuwa wanawake wanaoishi na VVU nchini wenye umri kati ya miaka 45 hadi 49 ni asilimia 12, huku upande wa wanume wenye umri wa miaka kati ya 40 hadi 44 ni asilimia 8.4.

“Ukiangalia upande wa Vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wanaoishi na VVU ni asilimia 2.1 kwa wasichana na asilimia 0.6 kwa wavulana.

“Utaona kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU kwa wanawake wenye umri kuanzia 15-39 ni mara mbili ya wanaume wenye miaka 15 hadi 39,” anasema Kitula.

Hii ni sawa na kusema kwamba katika kila kundi la wanawake wanne basi mmoja kati yao anaishi na maambukizi ya VVU.

Hali ya VVU duniani

Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu wanaokadiriwa kuwa milioni 1.7 (milioni 1.2-2.2 milioni) ambao walipata VVU ulimwenguni mnamo 2019 walionyesha kupungua kwa asilimia 23 kwa maambukizo mapya ya VVU tangu 2010.

“Ulimwenguni, idadi ya kila mwaka ya maambukizo mapya imekuwa ikishuka kwa kasi zaidi kati ya wanawake na wasichana (kupungua kwa asilimia 27 tangu 2010) kuliko wanaume na wavulana ambao kasi ya kupungua ni asilimia 18.

“Kulikuwa na maambukizo mapya machache mwaka 2019 ulimwenguni kati ya wanawake na wasichana (asilimia 48 ya jumla ya maambukizo) kuliko wanaume na wavulana (asilimia 52).

Aidha, kwa mujibu wa Kitula, mwaka 2019 kulikuwa na maambukizo mapya machache ulimwenguni kati ya wanawake na wasichana ambayo ilikuwa asilimia 48 ikilinganishwa na wanaume ambayo ilikuwa asilimia 52.

Watoto wenye umri kati ya miaka 0 hadi 14 walichangia asilimia 9 ya maambukizo mapya mwaka 2019 huku asilimia 84 ya maambukizo ya watoto yakitokea Kusini na Mashariki mwa jangwa la Sahara.

Hii ni sawa na kusema kwamba kiudini mwa Jwanga la Sahala ndiko kuliko na changamoto zaidi ya maambukizi ya VVU ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani.

Huduma za VVU nchini

“Asilimia 65.2 ya watu wazima wenye umri wa miaka 15 na kuendelea waliripoti kuwa wamewahi kupima VVU ambapo kati yao (asilimia 59.2 ni wanaume na asilimia 70.8 ni wanawake).

“Kwa ujumla asilimia 31.3 ya watu wazima wenye umri wa miaka 15 na kuendelea waliripoti kuwa wamepimwa VVU katika miezi kumi na mbili iliyopita kabla ya utafiti kufanyika ambapo asilimia 29 ni wanaume na asilimia 33.5 ni wanawake.

“Pia Asilimia 15.7 ya waliopima na kugundulika na VVU hawakuwahi kupima VVU kabla ya utafiti.

ambapo asilimia 19.7 ni wanaume na asilimia 13.7 ni wanawake,” anasema Kitula.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img