1.4 C
New York

Infographic| Mabegi yanavyoacha maumivu kwa wanafunzi

Published:

Kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kawaida kukutana na wanafunzi hususan wa elimu msingi wakiwa na mabegi makubwa mgongoni wakati wa kwenda na kurejea kutoka shule.

Aidha, mzigo mkubwa wanaonekana kuwa nao wanafunzi wanaosoma katika shule za binafsi ambao huonekana na mabegi makubwa bila kujali umri wao.

Wapo baadhi watu ambao huwatupia lawama walimu kwa wakubebesha mabegi na vitabu ambavyo wakati mwingine hudhaniwa kuwa havitumiki vyote kwa siku husika.

Flora Joshua ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam ni mama wa watoto wawili ambapo anasema kuwa mmoja wa watoto wake anayemtaja kwa jina la Christopher(6) anayesoma darasa nne ambaye amekuwa akilalamikia maumivu ya miguu na mgongo mara kwa mara.

“Hii ya mabegi mimi kama mzazi nakiri kwamba ni changamoto kwani mwanang mimi anavyorudi amekuwa akilalamika juu ya kuumwa mgongo na miguu na hiyo nikutokana na uzito wa mabegi wanayobeba wakati wa kwenda shule.
“Ali ana umri wa miaka sita pekee ninaamini chanzo cha maumivu anayolalamika mara kwa mara yanatokana na begi zito la shule analobeba.
“Mikoba ya shule ni mizito sana siku hizi. Hata mimi siwezi kuinua begi la mtoto wangu,” anasema Flora.
Hoja hiyo inaungwa mkono na wazazi wengine wanaonyoshea kidole uzito wa mikoba ya wanafunzi kuwa tishio kwa usalama wa afya za watoto.

Helena Mussa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Kwigutu iliyoko wilayani Butiama mkoani Mara, anasema: “Shule zinapaswa kupunguza idadi ya vitabu ambavyo wanafunzi wanapaswa kubeba. Kwa sasa kila somo lina nakala zipatazo tatu na vitabu viwili na watoto wanatakiwa wavibebe vyote.

“Ninafikiri shule zinapaswa kuwa na makabati ya wanafunzi ambayo wanaweza kuweka vitabu vya ziada,” anasema.

Tabibu wa binadamu, Dk. Nicolaus Magesa, anabainisha kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake, ameshuhudia ongezeko la watoto wenye umri wa kati ya miaka 14 na 17 wakilalamika juu ya maumivu ya mgongo, hasa eneo la chini la mgongo.

Anasema moja ya sababu waliyobaini inachangia kuwapo kwa shida hiyo ni mifuko na mabegi mazito ya shule wanayobeba wanafunzi.

Mbali na uzito wa mabegi na mifuko hiyo, Dk. Magesa amesema ufuatiliaji wao umebaini maumivu hayo pia yanachagizwa na mkao mbaya wa wanafunzi.

“Mkoba mzito wa shule unaathiri kiafya lakini athari zake huenda zisionekane haraka, lakini zikaja kuonekana baadaye maishani.

“Watoto siku hizi wanabeba mifuko mizito ya shule migongoni mwa, uzito huo utavuta mwili. Ili kulipa fidia, mwili unasonga mbele ili kuweka usawa fulani,” anafafanua.

Dk, Magesa anasema kuvutwa huko kwa mwili kusababisha maumivu kwa kuwa uzani wa begi unakuwa umezidi uzito wa mwili au eneo viungo husika vya mwili vilivyobeba uzito huo.

Ubebaji wa mabegi makubwa miongoni mwa wanafunzi, ni utamaduni unaoonekana kuchipuka nchini katika miaka ya karibuni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img