20.4 C
New York

Ukuaji wa Shughuli za Uchumi, Robo ya Pili ya Mwaka 2021

Published:

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2021, Shughuli ya Habari na Mawasiliano nchini ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 12.3 ikifuatiwa na Uzalishaji Umeme (asilimia 12.1).

Huduma nyingine za jamii zinazojumuisha Sanaa na Burudani; na shughuli za Kaya katika kuajiri (asilimia 10.8); Malazi na Huduma za Chakula (asilimia 10.1); Usambazaji Maji (asilimia 8.4) na Uchimbaji madini na mawe (asilimia 7.3).

Mchango katika Kiwango cha Ukuaji, Robo ya Pili Mwaka 2021

Aidha, shughuli zote za uchumi zilizofanyika katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2021
zilichangia ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha asilimia 4.3 ikilinganishwa na
asilimia 4.0 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Shughuli za uchumi zilizokuwa na mchango mkubwa katika ukuaji huo zilikuwa ni pamoja na: Kilimo (asilimia 13.0), Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo (asilimia 8.4) Biashara na Matengenezo (asilimia
8.1), Chimbaji Madini na Mawe (asilimia 7.6); Uzalishaji Viwandani (asilimia 7.6)
Ujenzi (asilimia 7.1) na Habari na Mawasiliano (asilimia 5.2).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img