1.4 C
New York

Visualization| WaterAid inavyojali afya, usafi Dar es Salaam

Published:

KATIKA kuadhimisha Siku ya Kunawa Mikono Duniani, shirika lisilo la kiserikali la WaterAid Tanzania, limekabidhi vituo 12 vya kunawia mikono kwenye maeneo tofauti jijini Dar es Salaam ikiwa ni kati ya vituo 35 ilivyotoa nchi nzima kufikia sasa.

Shirika hilo lenye makao makuu nchini Uingereza, limetoa vituo hivyo kwa kushirikiana na The Foreign, Commonwealth &Development Office(FCDO) na Uniliver ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kusaidia Watanzania kunawa mikono kupambana na magonjwa ya kuambukiza ikiwamo Uviko-19.

Hafla ya kuzindua vituo hivyo ilifanyika Oktoba 15,2021 ambayo ni siku ya maadhimisho ya kunawa mikono duniani katika Hospitali ya Mwananyamala, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘Maisha Yetu Yako Mikononi Mwetu, Tutembee Pamoja’.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkaazi wa WatarAid Tanzania, Anna Mzinga, ametaja maeneo ambayo wameweka vituo hivyo vya kunawia mikono kuwa ni ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Hospitali ya Mwanyamala, Hospitali ya Manzani Mmoja, Hospitali ya Temeke,Kituo cha Magufuli, Shule za msingo Malamba Mawili, Msasani na kituo cha daladala cha Mawasiliano.

Anna ametoa wito kwa Serikali, kutoa kipaombele katika miundombinu ya usafi wa mikono kwenye vituo vya huduma za afya, shuleni na maeneo ya umma pamoja na uwepo wa miradi ya usafi.

“Pasipo na huduma sahihi za maji, usafi wa mazingira na vifaa vya kunawia mikono katika makazi, shule, vituo vya kutolea huduma za afya na taasisi nyingine basi mazingira yetu yatakuwa ni vyanzo vya magonjwa na kuacha jamii katika hatari ya kupata milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na kuiningia gharama kubwa ya matibabu na kupoteza nguvu ya uzalishaji.

“Ukiondoa afua nyingine, wote ni mashahidi namna unawaji mikono umeongezeka nchini kwa kila sehemu ya biashara, taasisi na makazi kwa kuweka vifaa vya kunawia, maji na sabuni. Utaona Taifa tulivyopambana na Uviko 19 kupitia unawaji mikono,” – Anna.

“Ukiondoa afua nyingine, wote ni mashahidi namna unawaji mikono umeongezeka nchini kwa kila sehemu ya biashara, taasisi na makazi kwa kuweka vifaa vya kunawia, maji na sabuni. Utaona Taifa tulivyopambana na Uviko 19 kupitia unawaji mikono,” – Anna.

Anna Mzinga

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Rashid Mfaume mbali na kuipongeza WaterAid anasema kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Mfaume anasema maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na kijikinga dhidi Uviko 19 na kuanzia sasa huduma huduma sahihi za afya lazima kuzingatia upatikanaji wa maji.

Unawaji mikono ngazi ya Kaya

Mwaka201920202021(Sept)
Kaya zenye vifaa vya kunawia mikono332,3281,060,0611,152,868
Kaya zenye vifaa vya kunawia mikono pamoja na sabuni 291,8701,003,2221,200,963

Maeneo ya kutoa huduma za Afya

Mwaka20202021 hadi Sept
Maeneo ya kutoa huduma za Afya yenye vifaa
vya kunawia mikono
4151,020
Maeneo ya kutoa huduma za Afya yenye vifaa
vya kunawia mikono pamoja na sabuni
4041,012

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img