1.4 C
New York

Visualization: Kilimo kinavyohatarisha mazingira

Published:

SEKTA ya kilimo imekuwa na tija kubwa kwa maendeleo ya nchi nyingi barani Afrika, ikiwamo Tanzania.

Huku kikiwa chanzo cha ajira kwa asilimia zaidi ya 70 ya Watanzania, ni wazi kilimo kinastahili kuitwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii.

Ni kutokana na hilo, Serikali imekuwa na juhudi za makusudi kuimarisha sekta hii na moja kati ya hizo ni kile kinachofahamika kwa jina la Sensa ya Taifa ya Kilimo (NSCA).

Mwishoni mwa Mwaka wa Kilimo 2019-20, Serikali iliendesha Sensa hiyo ikilenga wakulima wadogo na wakubwa kote nchini na kubaini kuwa kati ya kaya 12,007,839 zilizopo nchini, 7,837,405 (65.3%) zinajihusisha na kilimo.

Kuni, mkaa kimbilio la wengi

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Sensa hiyo, bado jamii za wakulima zimekuwa mstari wa mbele katika uharibifu wa mazingira kwa kuwa zimeendelea kutegemea kuni na mkaa katika shughuli mbalimbali.

Ndiyo, wakulima 6,324,643 (80.7%) wanatumia kuni kwa ajili ya kupika. Katika idadi hiyo, wakulima wa Tanzania Bara ni 6,172,984, sawa na asilimia 80.6%, wakati wale wa Zanzibar ni 151,659 (84.2%).
Gesi inahitaji nguvu zaidi

Katika hatua nyingine, utafiti ukaonesha kuwa ni asilimia 2.3 pekee, kwa maana ya wakulima 181,193, ndiyo wanaotumia gesi ya viwandani katika shughuli za kupika.
Juu ya idadi hiyo, 178,543 (2.3%) ni wakulima wa Bara, huku 2,650 (1.5%) wakiwa ni wenzao wa Visiwani Zanzibar.

Zaidi ya hapo, utafiti umeeleza kwamba asilimia 2.2 ya jamii za wakulima nchini hutumia vyanzo vingine vya nishati na hapo unazungumzia umeme, mafuta ya taa, vinyesi vya mifugo, gesi asilia n.k.

Nini kifanyike?

Kama ilivyoainishwa na utafiti, kiwango kikubwa hicho cha utumizi wa kuni na mkaa ni kielelezo cha uhitaji wa nishati-safi kama vile umeme na gesi.

Ikimaanisha, utafiti huo ni fursa kwa Serikali kufanya mambo mawili makubwa. Mosi, kuendeleza mikakati ya kufikisha nishati ya umeme na gesi za viwandani katika maeneo mengi, hasa ya vijijini ambayo ndiyo yanayojishughulisha zaidi na kilimo.

Pili, jitihada za kufikisha nishati hizo vijijini ziende sambamba na elimu juu ya athari za ukataji miti unaotokana na uhitaji wa kuni na mkaa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img