1.6 C
New York

Infographic| Mwenendo wa chanjo ya corona nchini, elimu zaidi yahitajika

Published:

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto hadi kiufikia Jumamosi Agosti 28, 2021 jumla ya walengwa 304,603 wamepatiwa chanjo kwa hiari iliyoanza kutolewa hivi karibuni katika vituo vya kutolea huduma zaidi ya 550 kwa Tanzania bara.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili Agosti 29, na Wizara ya Afya kupitia kwa Katibu Mkuu, Prof. Abel Makubi, juu ya maendeleo ya utoaji wa chanjo ya UVIKO- 19 kwa Wanananchi,

Tathimini ya zoezi la utoaji chanjo tangu Mikoa yote izindue Agosti 4, 2021 inaonesha mpaka kufikia Agosti 28, jumla ya walengwa 304,603 wamepatiwa chanjo hiyo kwa hiari.

Kati ya hao waliopatiwa chanjo hiyo, walengwa 201,476 sawa na asiliamia (66.1) ni Wanaume na 103,127 sawa na asilimia (33.9) ni Wanawake.

“Ili kuongeza kiwango cha kasi ya wananchi kupatiwa huduma hii ya chanjo pasipo usumbufu naendelea kuelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri , kuhakikisha kuwa idadi ya vituo vinavyotoa chanjo vinaongezwa na kuanzisha huduma mkoba ili kutoa urahisi zaidi wa wananchi kupata chanjo pasipo usmbufu wakusafiri umbali mrefu.

“Pia katika vituo vyote, watoa huduma wote waendelee kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kila mteja watakaye mhudumia kwa magonjwa mengine ili kumpa nafasi ya uelewa na baadae yeye kuchukua maamuzi sahihi juu ya chanjo. Pia wananchi wanaofika kuchanjwa, wapewe elimu zaidi ya chanjo Pamoja na kufahamu hali zao za kiafya na maudhi ya kawaida ambayo yanaweza kutokea kwa baadhi ya wachache,” amesema Prof. Makubi.

Aidha, wizara hiyo imeziagiza mamlaka za mikoa, wilaya na mitaa kuhamsisha zoezi la chanjo ikiwa ni Pamoja na kuwepo kwa juhudi zaidi za kuongeza kasi katika maeneo ya pembezoni mwa ya miji na vijijini.

Wananchi pia wamekumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari zote za kkujikinga na Uviko -19.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img