8 C
New York

Visualization| Mitihani Darasa la Saba na ongezeko la watahiniwa

Published:

KESHO jumla ya wanafunzi 1,132,143 wataanza mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi (PSLE) kwa mwaka huu na idadi hiyo inatokana na shule 17,585 zilizoko nchini.

Aidha, kati ya idadi hiyo ya watahiniwa waliosajiliwa, wavulana ni 547,502 (48.36%) na wasichana ni 584,641 (51.64%), kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Charles Msonde.

Wakati huo huo, watahiniwa 1,079,943 (95.39%) watafanya mitihani ya lugha ya Kiswahili, huku 52,200 (4.61%) wakifanya kwa Kiingereza. Kwamba idadi ya wanaotumia Kiswahili imepanda, ukilinganisha na mwaka jana walipokuwa 974,532. Kwa upande wa Kiingereza, idadi imepungua kwani mwaka jana walikuwa 49,475.

Kwa upande mwingine, watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 3,327, ambapo 108 ni wasioona, 951 wana uoni hafifu, 739 ni viziwi, 358 wana matatizo ya afya ya akili, huku 1,171 wakiwa na ulemavu wa viungo vya mwili.

Pia, mwaka huu kuna ongezeko la watahiniwa 101,193 (10.57%), ulikinganisha na mwaka jana (1,029,950), kama ambavyo idadi ya masomo imepanda kutoka matano hadi sita (Uraia na Maadili limeongezeka).

“Pia, masomo mawili yameboreshwa maudhui yake hivyo somo la Sayansi litaitwa Sayansi na Teknolojia na somo la Maarifa ya Jamii litaitwa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img