7.1 C
New York

Visual| Tunayofahamu kuhusu Ikulu mpya ya Chamwino

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Mei 20, 2023 Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alizindua Ikulu mpya ya Chamwino mkoani Dodoma kama ofisi na makazi rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikulu hiyo imejengwa na Jeshi la Kujenga Taufa kupitia kitengo chake cha Uzalishaji mali-Suma JKT huku ubunifu na ujenzi wake ikisimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu hiyo, Dk. Samia alisema kuwa, utekelezaji wa mradi huo ni matokeo ya dhamira kuu ya Serikali ya kuhamia Dodoma.

Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi ulifikiwa katika Mkutano Mkuu wa 16 wa TANU uliofanyika mwaka 1973. Zaidi angalia usanifu wetu hapa chini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img