8.8 C
New York

Mitindo ya nywele kwa wanawake wenye vipara usoni

Published:

NA BRIGHITER MASAKI, DAR ES SALAAM

Nywele zilizonakishiwa ni moja wapo ya alama inayotambulisha urembo wa Mwanamke husika.

Kuna namna nyingi za kunakshi nywele zako, wapo wanaosuka mitindo tofauti au wanaopunguza kisha kuziongezea mvuto kwa njia tofauti.

Lakini wako pia ambao huzisuka bila kuweka dawa na kuzibana kwa mitindo tofauti.

Hata hivyo, kwa wanaopendelea kusuka, baadhi ya watu wamekumbana na changamoto ya kuwa na upara usoni na kusababisha nywele kukosa mvuto.

Wengine wameamua kukata nywele zao na wengine wakijaribu kutumia dawa tofauti tofauti kwa lengo la kuzirudisha katika mwonekano wa awali.

Wengi wamekuwa wakiendelea kusuka lakini wakipaka jeli usoni. Kumbuka unaweza kuendelea kuwa mrembo bila kukata nywele zako kwa kusuka mitindo tofauti ya kufunika upara usoni.

Unaweza kusuka rasta za vitunguu kisha ukazibana kwa namana ambayo nywele nyingine zitakunjwa upande wa usoni au kusuka yeboyebo kwa mtindo wa kuleta mbele nywele katika sehemu iliyoathiriwa.

Aidha, unaweza pia kushonea au kuvaa wigi kwa mtindo ambao nywele nyingine zitafunika sehemu ya usoni ambayo ni kipara.

Jambo la kuzingatia unapokwenda kwa msusi unatakiwa kumwambia akusuke kulingana na uso na nywele zako zilivyo huku akizingatia zile sehemu ambazo zimehathiriwa (zenye upara) kwa sababu wapo ambao wana upara utosini pembeni ya utosi na wengine sehemu za chini kuzunguka kichwa na wengine katikati ukisuka mtu awezi kugundua.

Kwa makala zaidi kuhusu urembo na mitindo endelea kutembelea tovuti yetu mara kwa mara.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img