10.6 C
New York

Ugumu wa maisha wazitikisa Ubelgiji, Italia, Ureno na Ufaransa

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MAANDAMANO makubwa yameshuhudiwa katika mitaa ya nchi mbalimbali za Ulaya, yote yakiwa na ajenda moja; kilio cha wananchi juu ya kupanda kwa gharama za maisha.

Jumamosi ya wiki hii, Oktoba 17, 2026, yalichomoza maandamano ya aina hiyo nchini Ubelgiji, wakati huo pia yakionekana katika mataifa ya Ufaransa, Italia na Ureno.

Nchini Ufaransa, maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 10 ya hivi karibuni yalihusisha wananchi zaidi ya 550,000, ambapo polisi walilazimika kuingilia kati ili kutuliza vurugu.

Kwa upande wa Ubelgiji, wananchi katika miji ya Brussels, walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kutawanya waandamaji. Ni wiki chache tu tangu wanafunzi walivyoandamana kupinga gharama kubwa za kujiunga na elimu ya juu.

Ureno nako hali ilikuwa ya aina hiyo katika Mji Mkuu wa Lisbon. Wananchi waliingia mitaani kuikosoa Serikali kwa kile walichoeleza kuwa imeshindwa kudhibiti ugumu wa maisha.

Wengi walieleza kukerwa na kupanda kwa gharama za kodi za nyumba, ambazo sasa ni mara mara mbili ya ilivyokuwa mwaka 2017.

Huko nchini Italia nako hali haikuwa tofauti. Miji mikubwa ya Milan na Bologna ilishuhudia purukushani za waandamanaji waliokuwa wakiwarushia mawe polisi waliojaribu kuwazuia.

Wakati huo huo, huenda ni suala la muda tu kushuhudia Ugiriki, Ujerumani na Austria nazo zikiingia kwenye maandamano ya raia wanaokazwa na kupanda kwa gharama za maisha.

Related articles

Recent articles